Search This Blog

Tuesday, February 9, 2021

Makofi ya wabunge yamchanganya Spika Ndugai


Spika wa Bunge Job Ndugai amesema baadhi ya wabunge wamekuwa wakipiga makofi bungeni lakini haijulikani wamepiga ya nini.


Ndugai alisema hayo jana wakati Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Khamis Hamza Khamis akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalumu (CCM) Husna Sekiboko kwamba polisi wamekuwa wakishindwa kufika kwa wakati maeneo mbalimbali kwa sababu ya kukosa mafuta na matengenezo ya magari.


Awali, akijibu swali Khamis alisema kwa mujibu wa sheria ya bajeti wenye fungu ni mkuu wa polisi nchini (IGP) na Ma-RPC hivyo fungu likitoka kwa IGP linakwenda kwa RPC na kisha kugawiwa kwa wakuu wa polisi wa wilaya husika.


Alisema wanalichukua suala hilo na kwenda kukaa na wadau ili kuona namna wanavyoweza kulifanyia mabadiliko.


Hata hivyo, majibu hayo yaliwafanya baadhi ya wabunge kumpigia makofi naibu waziri huyo, hali iliyomuibua Ndugai ambaye alisema kuna wakati wabunge wanapiga makofi haifahamiki wanapiga ya nini.


Ndugai alihoji kuwa: “Halafu waziri akakae na wadau, wakina nani? Halafu tunashangilia (wabunge) tunakubali hiyo kanzu.”



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...