Search This Blog

Tuesday, February 2, 2021

Mamia wakamatwa baada ya mpinzani wa Putin kufungwa


Watu wapatao 1,400 wamekamatwa nchini Urusi wakati wa maandamano yaliyotokea siku ya Jumanne baada ya kiongozi wa upinzani Alexei Navalny kufungwa, taarifa zinaeleza.

Kumekuwa na matukio ya vurugu huko Moscow - picha za video kwenye mitandao ya kijamii inaonesha polisi wakiwapiga na kuwakamata waandamanaji ambao walikuwa wanamuunga mkono Navalny.

Awali Bwana Navalny, 44, alifungwa miaka mitatu na nusu kwa kukiuka masharti ya hukumu aliyokuwa amepewa.

Alisema kesi dhidi yake ilikuwa haina ukweli wowote.

Alirudi Urusi mwezi Januari baada ya kupata matibabu nchini Ujerumani baada ya kunyweshwa sumu mwezi Agosti.

Bwana Navalny anasema Rais wa Urusi Vladimir Putin alitoa agizo la yeye kushambuliwa kwa kuekewa sumu ya Novichok, alimuelezea kuwa ni muuaji ingawa madai hayo yalikanushwa.

Umoja wa Ulaya, Marekani na Uingereza wamepinga vikali kifungo cha kiongozi huyo wa upinzani na kutaka aachiwe huru haraka.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...