Search This Blog

Tuesday, February 2, 2021

Baraza la madiwani Sikonge lapitisha makisio ya bilioni 28.3 za bajeti ya mwaka ujao wa fedha


BARAZA la Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge limepokeana limepitisha makisio bajeti ya mwaka wa fedha wa 2021/22 ya shilingi bilioni 28.3.

Kauli hiyo imetolewa na jana na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Rashid Magope wakati kikao cha Baraza la Madiwani cha Bajeti.

Alisema kati ya fedha hizo shilingi bilioni 20.1 ni matumizi ya kawaida  na miradi ya maendeleo ni bilioni 8.2.

Aidha Mwenyekiti huyo alisema katika mwaka ujao wa fedha Halmashauri hiyo wanakusudia kukusanya shilingi bilioni 3.2 kutoka vyanzo vyake vya ndani vya mapato.

Alisema kuwa bajeti ya mwaka ujao imepanda kwa asilimia 11.7 ukilinganisha na bajeti ya mwaka wa fedha wa 2020/21 ya shilingi bilioni 25.3.

Magope alisema bajeti ya mwaka ujao imejikita katika vipaumbele vya kukuza uchumi na maendeleo ya viwanda , kuimarisha miundombinu ya elimu, afya , kujenga skimu za umwagiliaji wa kilimo cha mpunga katika bonde la Kalupale lenye ukubwa hekta 2,008.

Aliongeza kuwa vipaumbele vingine ni uanzishaji wa mashamba makubwa ya kilimo cha mazao ya kudumu kama vile miembe na korosha, kukamilisha jengo la Utawala la Halmashauri, ujenzi wa viwanda vidogo na kukatua kero za wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri alisema bajeti ijayo ni vema ikajikita katika uimarishaji wa kilimo cha mashamba makubwa ambayo yatawawezesha kuzalishaji mazao mengi ambayo yatawawezesha kuwa na fedha nyingi za kujitegemea kwa asilimia 100.

Aliongeza ni vema wakahakikisha kuwa kunakuwepo kwa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo na asilimia 10 kwa ajili ya vikundi vya wanawake , vijana na watu wenye ulemavu.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka Madiwani kushirikiana na watendaji na jamii katika kuhamisha wanafunzi wa madarasa ya mitihani kuweka kambi za maandalizi ya mitihani ya kitaifa ili kuinua ufaulu.

Alisema hatua hii inakwenda sanjari na mapambano dhidi ya utoro sugu miongoni mwa wananfunzi ikiwemo kuwachukulia hatua wahusika kwa mujibu wa Sheria zilizopo.

Aidha Magiri alimwagiza Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Sikonge kuendesha opresheni ya kumata watoto wote watakaokutwa wakicheza kamali na mabonaza wakati wa masomo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...