Search This Blog

Tuesday, February 2, 2021

UWT Manyara watoa neno kuhusu urithi wa kiti cha Mbunge aliefariki


Na John Walter-Manyara

Jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania ya CCM (UWT) Mkoani Manyara, imedai kuwa bado wanasubiri utaratibu kutoka makao makuu juu ya mchakato wa kumpata mrithi wa marehemu Martha Umbulla aliyekuwa mbunge wa Vito maalum.

Katibu wa UWT Mkoani Manyara, Highnes Munisi aliyasema hayo  mjini Babati akizungumza juu ya mchakato wa mrithi wa marehemu Mbunge huyo.

Munisi alisema wao kama UWT ngazi ya mkoa hawana cha kuzungumza juu ya hilo zaidi ya kusubiri muongozo kutoka UWT ngazi ya Taifa na CCM kwa ujumla.

"Utaratibu utakaotumika kupata mtu wa kurithi nafasi hiyo tunasubiria ila sisi tulimaliza kazi yetu kwa wagombea ubunge 42 waliogombea viti maalum na kuwapata watatu," alisema Munishi.

Alisema hawezi kuzungumza zaidi juu ya hilo kwani bado wapo kwenye majonzi ya kuondokewa na mbunge huyo wa viti maalum kwenye mkoa huo.

Hata hivyo, alitoa pole kwa wanawake wote wa jumuiya hiyo kwa kuondokewa na mbunge huyo ambaye alikuwa kiungo na  wa mfano kwa wanawake wote.

Alisema wanamshukuru Mungu kwa kuwapa nafasi ya kuwa na mbunge huyo ambaye alitumikia nafasi hiyo ipasavyo ila kazi ya Mungu haina makosa.

"Tumepata funzo kupitia mama Umbulla kuwa ukipata fursa itumike kwa nguvu na uwezo wako wote ili mwisho wa siku wengine wapate elimu kuwa kuwatumikia watu ni kipaji hivyo kitumie," alisema.

Marehemu Umbulla alifariki dunia nchini India wakati akipatiwa matibabu Januari 21 mwaka huu na kuzikwa nyumbani kwake kata ya Dongobesh wilayani Mbulu Januari 26.

Marehemu Umbulla alishika nafasi hiyo kwa miaka 16 mfululizo tangu mwaka 2005 alipochaguliwa kwa mara ya kwanza na miaka yote huwa anaongoza kwa kushika namba moja.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...