Search This Blog

Thursday, February 18, 2021

Maambukizi ya COVID-19 yamepungua duniani


Shirika la Afya Duniani, (WHO) limesema kwamba idadi ya visa vipya vya virusi vya corona vimepungua kwa asilimia 16 ulimwenguni wiki iliyopita. WHO imesema kuwa takwimu hizo zimepungua kwa visa 5,000,000 hadi milioni 2.7.

Wiki ya kwanza ya Januari, visa vipya vya corona viliongezeka kwa takriban milioni 5. Wiki iliyopita karibu maeneo yote ulimwenguni yalishuhudia kupungua kwa maambukizi ya COVID-19, isipokuwa katika eneo la Mashariki ya Kati.

Pia idadi ya vifo vilipungua duniani wiki iliyopita, kwa vifo vipya 81,000, ambapo vimepungua kwa asilimia 10.

Kupungua kwa maambukizi ya virusi vya corona pamoja na vifo kunatokea wakati ambapo nchi nyingi zinaendelea kutoa chanjo.

Wakati huo huo, Afrika Kusini imeahidi kutoa dozi milioni moja za chanjo ya AstraZeneca kwa mataifa mengine ya Afrika na nchi hiyo imeamua kutumia chanjo ya Johnson & Johnson.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...