Search This Blog

Saturday, February 20, 2021

Kardashian 'awasilisha ombi kutalikiana na Kanye West'


Kim Kardashian awasilisha ombi mahakamani la kutalikiana na mwanamuziki wa rappa Kanye West, kulingana na taarifa za vyombo vya habari Marekani.

Wawili hao wameoana kwa karibu miaka saba na kujaaliwa watoto wanne pamoja.

Taarifa hizo zimejitokeza mara ya kwanza katika tovuti ya watu maarufu TMZ baada ya miezi kadhaa ya uvumi kuwa ndoa yao inayumba.

Taarifa katika vyombo vya habari vya Marekani zimesema nyota huyo wa kipindi cha televisheni, 40, ameomba kuruhusiwa kisheria kutunza watoto wao.

Hata hivyo, hakuna kati yao ambaye amezungumzia suala hilo hadharani.

Wanandoa hao ni miongoni mwa nyota wanaotambulika zaidi duniani na wote wamefanikiwa kwa kiasi kizuri katika kazi zao.

Mara ya kwanza Kim kuwa maarufu ni mwaka 2007 kama nyota wa kipindi cha televisheni kinachoonesha maisha ya uhalisia kuhusu familia yake cha 'Keeping Up With the Kardashians' ambacho bado kimeendelea kuwa maarufu huku mfululizo wa kipindi hicho kwa mara ya 21 na wa mwisho kikiwa kitaanza kupeperushwa hewani mwaka ujao.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...