Search This Blog

Saturday, February 20, 2021

Serikali yataja Chanzo kifo cha Balozi Kijazi chatajwa


Serikali imeweka wazi chanzo cha kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, na kusema kuwa amefariki kutokana na maradhi ya moyo na aliugua kwa muda mfupi.

Akisoma wasifu wa Marehemu Balozi Kijazi, Katibu Mkuu Utumishi Laurean Ndumbaro, amesema kuwa Balozi Kijazi, alizaliwa mkoani Mwanza akiwa ni mtoto wa pili kwenye familia ya watoto 10

"Balozi Mhandisi John Kijazi ameugua kwa muda mfupi ambapo februari 1 , 2021, alilazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma, hadi mauti yalipomfika na amefariki kwa maradhi ya moyo akiwa na miaka 60", amesema Dkt. Ndumbaro 

Marehemu Balozi Mhandisi John Kijazi ameacha mke, watoto watatu pamoja na wajukuu wawili, na atazikwa leo Februari 20, 2021, wilayani Korogwe mkoani Tanga



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...