Rais wa Benki ya Dunia David Malpass amesema taasisi hiyo inafanya kazi kwa pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kuangalia uwezekano wa kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa ili kuendeleza mazungumzo kwa lengo la kupunguza mizigo ya madeni kwa baadhi ya nchi masikini.
Nchi tatu za Afrika Ethiopia, Chad na Zambia tayari zimeanzisha mazungumzo na wadai wake chini ya mfumo mpya unaoungwa mkono na kundi la nchi za G20 zenye uchumi mkubwa. China,
Mearekani na nchi zingine za G20 awali ziliweka mchakato wa kusimamisha ulipaji wa madeni kwa muda kwa nchi masikini zaidi duniani.

No comments:
Post a Comment