Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa litakutana siku ya Jumanne kujadili changamoto za kisiasa nchini Somalia, Shirika la habari la Ufaransa, AFP limeripoti likinukuu vyanzo vya kidiplomasia.
Upinzani nchini Somalia umeapa kutomtambua Rais Mohamed Abdullahi Farmajo, ambaye muhula wake ulimalizika siku ya Jumatatu.
Bado haijajulikana uchaguzi utafanyika lini.
Mazungumzo kati ya serikali na majimbo kuhusu namna gani ya kufanya uchaguzi yalivunjika tarehe 5 mwezi Februari.
Kuepuka ombwe la madaraka, bunge lilipitisha azimio mwaka jana kumruhusu rais na bunge kuendelea na nafasi zao mpaka warithi watakapochaguliwa.
Umoja wa Mataifa umetaka viongozi wa nchi hiyo wafanye mazungumzo.
Nchi hiyo tayari ilikuwa kufanya uchaguzi wa bunge mwezi Desemba 2020 kwa sababu ya mizozo inayoendelea kati ya serikali na tawala zingine za mikoa.
No comments:
Post a Comment