Search This Blog

Tuesday, February 9, 2021

Waziri Mkuu wa Sudan ateua viongozi wa waasi kwenye serikali


Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok amelitaja baraza jipya la mawaziri ambalo linahusisha viongozi wa zamani wa waasi ambao walikuwa sehemu ya mkataba wa Amani uliosainiwa mwezi Oktoba.

Bw.Hamdok alivunja baraza lililopita siku ya Jumapili kwa ajili ya kuunda serikali ya umoja.

Mawaziri wawili walichaguliwa kutoka kwenye jeshi. Wengi kutoka kutoka kwenye vikosi vya Uhuru na mabadiliko vilivyoongoza maandamano yaliyomuondoa Omar al-Bashir madarakani.

Waziri Mkuu amemteua kiongozi wa zamani wa waasi na mwanauchumi Gibril Ibrahim kuwa Waziri wa fedha.

Hatua hii imekuja wakati ambapo kuna upungufu wa chakula na mafuta na kupanda na mfumuko wa bei.

Kuwa waziri wa mambo ya nje wa Sudan katika eneo lenye hali tete pia itakuwa mtihani mkubwa. Kazi hiyo ilikwenda kwa Mariam al-Sadiqal-Mahdi- binti wa waziri mkuu wa mwisho wa aliyechaguliwa kidemokrasia, Sadiqal-Mahdi.

Bado kuna wanajeshi katika baraza la mawaziri la Bwana Hamdok - ukumbusho wa ndoa ngumu kati ya wanajeshi na raia wakati Sudan inaendelea na kipindi cha mpito kuelekea demokrasia.






No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...