Nchi ya Uturuki imeingia siku ya nne kwenye mchakato wa utoaji chanjo ya corona (Covid-19) ambapo hadi kufikia sasa dozi za kwanza za chanjo ya CoronaVac zimeweza kutolewa kwa wahudumu wa afya zaidi ya 700,000.
Kufuatia mapendekezo ya Kamati ya Sayansi ya Corona na kulingana na "Mkakati wa Utekelezaji wa Chanjo ya Covid-19" uliowekwa na Wizara ya Afya, mchakato wa chanjo ulioanzishwa kote nchini siku ya Alhamisi, Januari 14, bado unaendelea. Katika muktadha huu, kwanza kabisa, wafanyikazi wa huduma ya afya walipewa chanjo.
Siku ya nne ya mchakato wa chanjo ambayo hadi kufikia sasa zaidi ya wafanya kazi 700,000 wa huduma za afya walipewa dozi za kwanza za chanjo ya CoronaVac iliyozalishwa na kampuni ya Sinovac.
Baada ya chanjo huyo kumalizika kutolewa kwa wahudumu wa afya 1,100,000 nchini Uturuki, wazee, walemavu, waangalizi, walezi wa vituo vya watu wasiojiweza na wafanyikazi wengine pia watapewa chanjo. Kikundi hiki kitafuatwa na watu wenye umri wa miaka 65 na zaidi.

No comments:
Post a Comment