Na Omary Mmgindo, Kibaha
JUMUIA ya Wanawake UWT Mkoa wa Pwani imewataka Madiwani wa kike
mkoani hapa kuandaa mashindano ya netiboli ili kuwaokoa watoto wa kike.
Hatua hiyo inalenga kuwapunguzia muda wa kushiriki o vilivyo nje ya maadili, ambapo watatumia michezo hiyo kujiweka vizuri kiafya na kiakili.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Farida Mgomi, akizungumza kwenye Baraza lililoandaliwa na Jumuia hiyo, likitumika pia kuwapatia elimu madiwani wapya, ambapo alisema michezo ya netiboli, kuruka kamba na mingine itawaondolea michezo yasiyokuwa na msingi.
"Michezo inasaidia kiafya m pia ina nafasi nzuri katika ajira, kwa miaka ya hivi karibuni vijana wetu wanapata ajira kupitia michezo, hivyo nasi tuandae netiboli na mingine ili watoto wetu waweze kushiriki," alisema Mgomi.
Aliongeza kwamba michezo ya watoto wa kike haina gharama kubwa ukilinganisha na mpira wa miguu ambapo wasichana wanashiriki, ambao una gharama kubwa ukilinganisha na netiboli na mingine.
"Niwaombe tuwekeni kipaumbele Fatima michezo kwani itawasaidia vijana wetu wasijiingize katika makundi yasiyokuwa na naadili" alisema Mwenyekiti huyo.
Alisema kwamba si vibaya mashindano hayo wakiyapatia majina yao ikiwa ni sehemu ya kujitangaza, na kwamba hata ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM inaelekeza hivyo.
"Niwaombe hili tulikee mikakati maalumu kwani itatusaidia sisi wazazi na walezi kuwaokoa vijana wasijiingize katika makundi, pia tutakuwa na muda wa kuzungumza nao," alimalizia Mgomi.

No comments:
Post a Comment