Uingereza iliacha kufuata sheria ya EU saa 23:00 GMT, baada ya mpango mbadala wa usafiri , biashara, uhamiaji na ushirikiano wa kiusalama kuanza kutekelezwa.
Boris Johnson alisema Uingereza ina " uhuru mikononi mwake" na uwezo wa kufanya vitu "Tofauti na bora" na sasa muda uliokuwa ukisubiriwa umekwisha .
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema Uingereza itasalia kuwa "rafiki na mshirika".
Mawaziri wa Uingereza wameonya kutashuhudiwa changamoto katika siku na wiki chache zijazo, wakati sheria mpya zitakapoanza kutekelezwa na mashirika ya Uingereza yanayofanya biashara na bara Ulaya yatakapoanza kukumbana na mabadiliko hayo.
Maafisa wamesisitiza mifumo mipya ya mipakani ''iko tayari'' kuanza kazi licha ya hofu ya mizigo kukwama bandarini.
Uingereza ilijiondoa katika muungano huo wa kisiasa na kiuchumi uliyo na nchi wanachama 27 miaka mitatu na nusu iliyopita baada ya raia wa Uingereza kupiga kura ya maoni mwaka 2016, maarufu Brexit.
Lakini iliendelea kufuata sheria za kibiashara za EU katika kipindi cha miezi 11 wakati pande hizo miili zilipokuwa zikishauriana kuhusu ushirikiano wao wa kibiashara wa siku zijazo.
Baada ya mazungumzo hayo kukamilika, mkataba wa kihistoria uliafikiwa mkesha wa Krismasi. Ulikuwa sheria siku ya Jumatano baada ya kuidhinishwa na bunge.
Chini ya sheria hilo mpya, alioanza kutekelezwa 24:00 CET, Wafanyabiashara wa Uingereza watafikia masoko ya ndani ya EU bila kulipishwa kodi, kumaanisha bidhaa zinazosafirishwa kati ya Uingereza na Ulaya hazitatozwa kodi.
Lakini inamaanisha nyaraka zaidi kwa wafanyabiashara na watu wanaosafiri kwenda nchi za EU wakati bado kuna kutokuwa na uhakika juu ya nini kitatokea kwa benki na huduma, ambazo ni sehemu kuu ya uchumi wa Uingereza.
No comments:
Post a Comment