Search This Blog

Saturday, January 30, 2021

Rais wa Italia atoa agizo la kufanyika mazungumzo ya kutafuta serikali mpya


Rais wa Italia Sergio Mattarella anatarajia mazungumzo kati ya washirika wa zamani wa serikali ya muungano yataumaliza mgogoro uliosababisha kuvunjika kwa serikali hiyo. 

Amempa jukumu kiongozi wa tawi la chini la Bunge, Roberto Fico, kuanzisha mazungumzo hayo. Hatua hiyo ni baada ya kujiuzulu aliyekuwa Waziri Mkuu Giuseppe Conte hapo siku ya Jumanne.

 Muungano wa serikali ya mrengo wa kati na kushoto aliouongoza ulivunjika mnamo Januari 13 wakati chama cha waziri mkuu wa zamani Matteo Renzi cha Italia Viva, kilipojitoa baada ya kuzuka mzozo kuhusu matumizi ya pesa za misaada za Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kupambana na janga la corona. 

Rais Mattarella amempa bwana Fico muda wa siku nne, kuona kama anaweza kufaulu kuleta upatanishi kati ya vyama hivyo vilivyokuwa kwenye serikali ya mseto iliyokuwepo.

 Kushindwa kukubaliana juu ya serikali mpya kunaweza kusababisha Italia kuingia kwenye uchaguzi wa mapema na kuzidisha mgogoro wa kisiasa nchini humo unaoweza kuudhoofisha uchumi wa Italia na pia juhudi za kukabiliana na janga la corona.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...