Search This Blog

Saturday, January 30, 2021

Akamatwa baada ya kumuweka mama yake kwenye jokofu nyumbani kwa miaka 10


Polisi nchini Japan wamemkamata mwanamke mmoja baada ya mwili wa mama yake kukutwa kwenye jokofu nyumbani kwake.

Yumi Yoshino, 48, amesema kuwa alimkuta mama yake akiwa amefariki kisha aliuficha mwili wake miaka 10 iliyopita kwa sababu '' hakutaka kuhama'' katika nyumba waliokuwa wakiishi mjini Tokyo, vyombo vya habari vimeripoti, vikinukuu maafisa polisi ambao hawakutajwa majina yao.

Hakukuonekana majeraha yoyote kwenye mwili ulioganda barafu, polisi wameeleza.

Mamlaka hawakuweza kuthibitisha muda na sababu ya kifo cha mwanamke huyo.

Mwili uliripotiwa kugundulika na mfanya usafi baada ya Bi. Yoshino kulazimishwa kuondoka katika nyumba hiyo kwa sababu ya kukosa kodi.

Mwili ulikuwa umekunjwa kiasi cha kutosha kuingia kwenye jokofu lenye barafu, polisi walisema.

Bi Yoshino alikamatwa katika hoteli mjini Chiba karibu na jiji la Tokyo, siku ya Ijumaa.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...