Search This Blog

Saturday, January 30, 2021

Umoja wa Ulaya watangaza taratibu kali kudhibiti mauzo ya chanjo dhidi ya corona

 


Umoja wa Ulaya umetangaza taratibu kali za kudhibiti mauzo ya chanjo za corona ambazo imesema ni mali ya raia wa umoja huo. Umoja wa Ulaya utakuwa na mamlaka ya kuzuia uuzaji wa chanjo nje ya jumuiya hiyo.

 Shirika la afya duniani WHO limeikosoa hatua hiyo lakini Umoja wa Ulaya umeeleza kuwa ni muhimu kuhakikisha kampuni za madawa zinatekeleza mikataba iliyoisaini.

Kuanzia hapo jana Umoja wa Ulaya utafuatilia na ikiwa itabidi utazuia kuuzwa kwa dawa hizo nje ya jumuiya hiyo. 

Uamuzi huo umesababishwa na mvutano kati ya Umoja wa Ulaya na kampuni ya madawa ya Uingereza na Sweden- AstraZeneca.

 Kampuni hiyo imesema haina uwezo wa kuiuzia Umoja wa Ulaya vichupa vya chanjo kwa mujibu wa mkataba wa uliofikiwa baina ya pande mbili hizo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...