Sylvestre Ilunga Ilunkamba amejiuzulu rasmi kama waziri mkuu wa Jamuhuri ya kisemokrasi ya Congo, na kuwasilisha barua yake kwa Rais Félix Tshisekedi.
Bw Ilunga, ambaye ni mshirika mkuu wa mtangulizi wa Rais Tshisekedi, Joseph Kabila, ameongoza baraza la mawaziri la serikali ya Muungano kwa miezi 15.
Waziri mkuu (kushoto) alikwenda katika ofisi ya Rais kuwasilisha barua ya kujiuzulu kwake kwa Bw Tshisekedi (Kulia)Image caption: Waziri mkuu (kushoto) alikwenda katika ofisi ya Rais kuwasilisha barua ya kujiuzulu kwake kwa Bw Tshisekedi (Kulia)
Hatahivyo wabunge walipitisha kura ya kutokuwa na Imani na serikali yakeJumatano wiki hii na akapewa saa 24 awe amejiuzulu.
Kujiuzulu kwake kunatoa fursa kwa Rais Tshisekedi ya kuwateua washirika wake kama mawaziri.
Hadi sasa, utendaji wa Bw Tshisekedi umekuwa ukidhibitiwa na, muungano alionao na Bw Kabila ambao uliafikiwa wakati alipoingia madarakani miaka miwili iliyopita.
Ushindi wake katika uchaguzi mwezi Disemba 2018 ulisifiwa kam wa kihistoria-ambapo kulikuwa na makabidhiano ya kwanza ya utawala kwa njia ya amani ambayo hayakuwahi kushuhudiwa katika historia ya miongo sita nchini humo.
Huu ndio mwisho wa muungano kati ya Bw Kabila na Bw TshisekediImage caption: Huu ndio mwisho wa muungano kati ya Bw Kabila na Bw Tshisekedi
Bw Tshisekedi bado hajamchagua waziri mkuu mpya,ambaye ataunda serikali ijayo.

No comments:
Post a Comment