Search This Blog

Tuesday, January 26, 2021

Rais Recep Tayyip Erdoğan azungumzia hatua zilizochukuliwa kuhusu chanjo ya virusi vya corona


Rais Recep Tayyip Erdoğan alisema kuwa hatua walizochukua kuhusu chanjo ya virusi vya corona (Covid-19) zimewezesha upatikanaji wa chanjo hizo kwa haraka.

Erdoğan alizungumzia suala hilo kwenye "Sherehe ya Uteuzi wa Kijamii" iliyoandaliwa katika Ikulu ya Rais.

Akibainisha kuwa miundombinu na nguvu kubwa za huduma zimeiwezesha Uturuki kujinasua katika kipindi hiki cha matatizo, Erdoğan alisema,

"Tumeweza kuona majaribio ya mfumo wetu wa misaada wa kijamii wakati wa janga. Hatukupata matatizo ya kiafya ambayo ingekatisha tamaa katika kipindi cha janga kilichodumu kwa takriban mwaka 1. Tulihakikisha nchi yetu ipo imara kwa malipo yetu ya kulinda jamii ya zaidi ya lira bilioni 46 na msaada tuliotoa katika eneo pana."

“Kuna uhaba wa chanjo katika nchi zilizoendelea zaidi duniani, hawawezi kupata. Tulianza kuagiza chanjo zetu kwa haraka. Kwanza kabisa, dozi milioni 50 za chanjo zitakuja nchini mwetu. Tumefanikiwa kuacha kipindi cha matukio ya kuvunja moyo nyuma zaidi kuliko hata katika nchi tajiri."



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...