Search This Blog

Tuesday, January 26, 2021

Tetesi za soka kimataifa

 


Klabu ya Tottenham imewasiliana na kiungo wa kati wa PSG na Argentina Angel di Maria kuhusu uhamisho wa kwenda London. Mchezaji huyo wa zamani wa Man United mwenye umri wa miaka 32 anapatikana kwa uhamisho wa bila malipo mwisho wa msimu huu. (L'Equipe via Talksport)

PSG bado inatumai kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham na England Dele Alli, 24, kwa mkopo kwa kipindi chote cha msimu kilichosalia . Spurs inafikiria kumsaini kiungo mchezeshaji wa Borussia Monchengladbach na Ujerumani Florian Neuhaus, 23, kama mtu atakeyechukua nafasi yake. (Mirror)

Spurs pia imehusishwa na uhamisho wa beki wa Napoli na Serbia Nikola Maksimovic, 29, ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho wa msimu huu. (Spazio Napoli via Sport Witness)

Thomas Tuchel amedaiwa kutopoteza muda katika mipango ya siku za usoni ya Chelsea kama mkufunzi wa klabu hiyo. Raia huyo wa Ujerumani ambaye alichukua mahala pake Frank Lampard katika uwanja wa Stamford Bridge siku ya Jumanne amesema beki wa klabu ya RB Leipzig na Ufaransa Dayot Upamecano, 22, ni miongoni mwa wachezaji anaowalenga sana. (SportBild via Team Talk)

Kufutwa kwa Lampard kumeiwacha klabu ya West Ham ikiwa na matumaini kwamba hamu ya Chelsea ya kumsajili mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 22 itakuwa imeisha. (Telegraph, subscription required)

Beki wa kushoto wa Chelsea Baba Rahman anatarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza kuondoka katika klabu hiyo tangu mkufunzi Lampard kupigwa kalamu , huku mchezaji huyo wa Ghana mwenye umri wa miaka 26, akitarajiwa kujiunga na klabu ya Ugiriki PAOK Salonika kwa mkopo. (Sport24 via London.Football)

Winga wa Manchester United Facundo Pellistri anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ya Old Trafford kwa mkopo huku Club Bruges na Alaves zikimnyatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 raia wa Uruguay, ambaye alijiunga na The Red devils kutoka Penarol mwezi Oktoba. (Goal)

Mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke, 30, anatarajiwa kusalia katika klabu ya Crystal Palace licha ya klabu ya West Bromwich Albion kumnyatia. (Sky Sports)

Leicester City ina matumaini ya kumsaini mchezaji iliokuwa ikimlenga kwa muda James Tarkowski kutoka Burnley mwisho wa msimu huu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amesalia na miezi 17 katika kandarasi yake na bado hajaamua iwapo atasalia na the Clarets ambao awali walikuwa wamekataa maombi kutoka kwa The Foxes na West Ham. (Mirror)

Arsenal ina kibarua kigumu cha kushindana na Barcelona katika kumsajili beki wa kati wa Manchester City mwenye umri wa miaka 21 Eric Garcia, ambaye anatarajiwa kuondoka kama mchezaji huru mwisho wa msimu huu. (Mundo Deportivo via Express)



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...