Search This Blog

Thursday, January 21, 2021

Moto katika kituo cha kuuguza wazee Ukraine


Watu 13 wamepoteza maisha  kwenye mkasa wa moto uliotokea katika kituo cha kuuguza wazee nchini Ukraine.

Katika taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Huduma ya Dharura ya Ukraine, iliripotiwa kuwa moto huo ulitokea kwenye kituo cha kuuguza wazee iliyoko katika mji wa Kharkov mwendo wa saa 15.50 nchini humo.

Taarifa zaidi zilieleza kuwa watu 13 walipoteza maisha na wengine  4 walijeruhiwa kutokana na  moto huo.

Mamlaka husika ilitoa maelezo na kusema kwamba kulikuwa na watu 33 ndani ya jengo hilo wakati wa moto.

Hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusiana na chanzo cha kuzuka kwa moto huo.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...