Shirika kubwa duniani la uzalishaji chanjo nchini India (Serum Instutute of India) limekumbwa na mkasa wa moto uliozuka katika jengo lake moja.
Moto huo umeripotiwa kuzuka katika jengo la shirika hilo ambalo lilikuwa kwenye hali ya ujenzi katika kwenye mji wa Pune katika jimbo la Maharashtra nchini India.
Mamlaka ilitangaza kuwa moto huo haukuathiri sehemu ya hifadhi ya chanjo lakini vyombo vya habari vya ndani vilichapisha picha zinazoonyesha moshi mkubwa ukitoka kwenye jengo hilo na wafanyikazi wakitoka nje na nguo zao za maabara.
Kuna wasiwasi kwamba moto huo ambao chanzo chake bado hakijajulikana unaweza kukatisha mipango ya taasisi hiyo ya kuongeza uzalishaji wa chanjo ya corona (Covid-19) katika siku zijazo.
Wazima moto ambao waliingilia kati kukabiliana na moto huo walitangaza kuwa watu 3 waliokolewa na hakuna yeyote aliyepoteza maisha.
Mamlaka ilisema kwamba moto huo haukuenea kwenye vituo ambavyo chanjo ya Covid-19 ilitengenezwa wala kuathiri hifadhi za vdozi milioni 50.
Afisa Mtendaji wa shirika hilo Adar Poonawalla alisema, "La muhimu zaidi hakukuwa na majeruhi au hasara mbaya katika mkasa wa moto."
Shirika la Serum of India ambalo ni la uzalishaji mkubwa wa chanjo ulimwenguni, limesaini makubaliano ya kutoa dozi bilioni moja za chanjo ya AstraZeneca / Chuo Kikuu cha Oxford.
Poonawalla alitangaza mwezi uliopita kwamba taasisi hiyo inakusudia kuongeza uwezo wake wa uzalishaji kutoka dozi bilioni 1.5 hadi dozi bilioni 2.5 kufikia mwisho wa mwaka 2021.

No comments:
Post a Comment