Search This Blog

Tuesday, January 26, 2021

Merkel na Biden wajadili changamoto za ulimwengu


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Marekani Joe Biden wamekubaliana jana kuwa hatua za pamoja zitasaidia kupambana na janga la virusi vya corona pamoja na changamoto nyingine zinazoukabiili ulimwengu. 

Katika mazungumzo ya kwanza kwa njia ya simu tangu Biden alipoapishwa kuiongoza Marekani, viongozi hao wawili wameafikiana kuwa juhudi za kimataifa ndiyo muhimu kwenye kukabiliana na vizingiti vinavyoiandama dunia. 

Bibi Merkel ameukaribisha kwa bashasha uamuzi wa Marekani wa kujiunga tena na shirika la afya duniani WHO na mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa mjini Paris na kumhakikishia rais Biden ushirikiano wa Ujerumani kwenye kutafuta majibu ya changamoto za kimataifa. 

wenye mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine viongozi hao wamejadili masuala ya mabadiliko ya tabianchi na biashara na Merkel amemwalika rais Biden kuitembelea Ujerumani muda ukiwadia.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...