Search This Blog

Tuesday, January 26, 2021

Yellen kuwa waziri wa fedha wa kwanza mwanamke nchini Marekani


Baraza la Seneti la Bunge la Marekani limepiga kura na kumuidhinisha kwa wingi mkubwa mwanauchumi anayeheshimika Janet Yellen kuwa waziri mpya wa fedha wa taifa hilo. 

Wajumbe wa Seneti wamemuidhinisha Yellen kwa kura 84 za ndiyo dhidi ya 15 za hapana na kumfanya kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza wizara ya fedha tangu ilipoanzishwa zaidi ya miaka 200 iliyopita.

 Yellen anatajwa kuwa miongoni mwa wachumi wenye tajriba kubwa baada ya hapo kabla kufanya kazi kama gavana wa benki kuu ya Marekani na mjumbe wa Baraza la washauri wa uchumi wa Ikulu ya White House. 

Katika hatua nyingine kamati ya masuala ya mambo ya kigeni ya Baraza la Seneti imemuidhinisha mwanadiplomasia mkongwe Antony Blinken kuwa waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani. Hatua hiyo inamsafishia njia Blinken yakuidhinishwa na Baraza la Seneti litakapopiga kura wiki inayokuja.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...