Search This Blog

Tuesday, January 26, 2021

Mamilioni ya Fedha yaokolewa mkoani Manyara,Magari, nyumba piki piki zarejeshwa kwa Wanyonge


Na John Walter-Manyara

Taarifa ya robo ya pili ya mwaka kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba 2020, Takukuru Manyara imefanikiwa kuwarejeshea waathirika wa mikopo umiza mali zao zikiwemo nyumba, piki piki na magari.

Mali hizo ambazo ni nyumba tano, pikipiki mbili na magari matatu ziliporwa baada ya kuingia mikataba ya kuchukua fedha kutoka kwa wakopeshaji ambao ilibainika wanakopesha kinyume na taratibu za sheria ya biashara ya fedha (The Microfinance Act, 2008) na kutozwa riba kubwa kinyume na taratibu.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari,Holle Makungu ambaye ni mkuu wa Takukuru mkoani Manyara amesema pamoja na wanyonge hao, walifanikiwakusaidia urejeshwaji wa mali nyingine zinazohusiana na mikopo umiza ambazo ni kiwanja cha Chama cha Mapinduzi ambacho kiliporwa tangu mwaka 2015 wilayani Kiteto chenye ukubwa wa 930.776m.

Makungu ameeleza kuwa katika wilaya ya Simanjiro walimsaidia mkurugenzi urejeshwaji wa shilingi Milioni 35,926,151.80 kutoka kwa wazabuni wakorofi huku ikiokoa kiasi cha shilingi Milioni 22,238,669.00 ambazo zilirejeshwa kutoka mikononi mwa watu wasiokuwa waaminifu waliokopeshwa kupitia vyama vya msingi ikiwa ni mikopo ya pembejeo za kilimo pamoja na kurejesha shamba lenye ukubwa wa ekari sabini kwa bibi Hando mwenye umri wa miaka 70 wilayani Kiteto.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...