Search This Blog

Tuesday, January 26, 2021

Maandamano yaibuka tena Tunisia baada ya kifo cha muandamanaji


Kumekuwa na maandamano mjini Sbeitla nchini Tunisia, yaliyochochewa na ripoti zilizotolewa kuwa kijana mmoja aliyejeruhiwa wakati wa mapambano ya wiki iliyopita amepoteza maisha akiwa hospitali.

Wanajeshi walisambazwa kwenye majengo ya serikali katia mji huo baada ya waandamanaji kujaribu kuvamia kituo cha polisi cha mji huo.

Familia ya mtu huyo, Haykel Rachdi, imesema aligongwa na mtungi wa gesi ya kutolea machozi.

Alijiunga na maandamano ya nchi nzima kuadhimisha kumbukumbu ya mapinduzi ya Tunisia, yaliyokaribisha demokrasia na kuchochea mapinduzi ya kiarabu katika ukanda huo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...