Search This Blog

Thursday, January 21, 2021

Mama Ndesi asaidia wanafunzi Mihande na Dosa Azizi


Na Omary Mngindo, Mlandizi

DIWANI wa Kata ya Mlandizi Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani Uephrasia Kadala, amewapatia madaftari makubwa wanafunzi 38 wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Akiambatana na Tatu Haji (Mwenyekiti wa UWT Kata) Rehema Kibwana na Glory Mshindo (Madiwani wa Viti Maalumu), wamepokelewa na mwenyeji wao Mwalimu Mkuu Azza Rashid, ambapo Kadala amesema lengo kuwawezesha Wanafunzi hao kushiriki masomo.

Kadala amewakabidhi wanafunzi 19 wa shule ya Mihande na 19 shule ya Dosa Azizi madafta makaunta book matatu mpaka manne kulingana na kidato chao, huku walimu kila shule wakikabidhiwa karatasi za kuchapishia mitihani.

"Nimeambatana na madiwani wenzangu Rehema Kibwana na Glory Mshindo wa Viti Maalumu washuhudie zoezi, lengo letu wanafunzi tuliowalenga waone ni namna gani tunavyoshirikiana nao katika kupambana na changamoto zinazowakabiri," alisema Kadala.

Kwa upande wake Kibwana alimpongeza mwalimu Azza kwa jitihada zake za kupambania elimu shuleni hapo, huku akizungumzia ufaulu ambapo alisema tangu afike shuleni hapo hali ya ufaulu na nidhamu inaridhisha.

Tatu Haji alisema kuwa Jumuia ya Wanawake UWT Kata itaendelea kuwa pamoja na shule hizo ili kuona walimu wanaendelea na kuwapatia elimu wanafunzi shuleni hapo, huku akiwaomba wazazi na walezi kuwaunga mkono.

Awali Mwalimu Azza alimshukuru Diwani huyo, huku akiwaomba wazazi na walezi kuwa na utatatibu wa kutembelea shule hatua itayowaongezea hamasa ya kufundisha walimu, huku akisema baadhi yao ni wageni maeneo hayo.

Nae Mwalimu Msaidizi shule ya Dosa Azizi Chadi Kasembe alisema kwamba upatikanaji wa makaunta hayo na karatasi za kuchapishia mitihani vitaongeza chachu ya elimu shuleni hapo, huku akiwaomba wadau wengine kuunga mkono juhudi hizo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...