Na Omary Mngindo, Chalinze
MKURUGENZI wa halmashauri ya Chalinze Mkoa wa Pwani Ramadhani Possi, amewatoa hofu viongozi wa Kijiji cha Lunga Kata ya Lugoba kuhusiana na kuhamishwa kwa Mtendaji wao Kervin Nchimbi, ambaye amehamishwa kijijini hapo.
Hofu hiyo inayosababishwa kukwama kwa mkutano wa kusomwa mapato na matumizi, imetolewa na Mwenyekiyi wa Kijiji hicho Elizabeth Masenga, akizungumza mbele ya Mkurugenzi huyo akiwemo Mbunge Ridhiwani Kikwete, ambapo alisema wananchi wanataka kusomewa maoato.
"Tunataka kusoma mapato na matumizi lakini kikwazo kinakuja kuhamishwa kwa Myendaji huyo, tumemwita mara kafhaa aje lakini amekuwa mkaidi huku wananchi wakilallamikia kitendo hicho wanahitahi kujua mapato yao na matumizi," alisema Elizabeth.
Akizungumza na ujumbe huo kuyoka kijijini humo ukionhozwa na Mwenyekiti huyo aliyeambatana na Diwani Rehema Mwene, Godbles Naibala, Karama Tamimu na viongozi mbalimbali, Possi aliwataka waandike barua kwake yeye atamruhusu aende.
"Mlivyokuwa mnawasiliana yeye hawezi kuja kwa utaratibu huo, niandikieni barua mkielezea madhumuni ya kumhitaji kwa ajili ya zoezi hilo, mimi nitamuagiza aje kwa ajili ya kufanikisha usomwaji wa mapato na matumizi ya kijiji," alisema Possi.
Aliongeza kwamba kwakuwa amehamisha kikazi kutoka kijijini hapo na kupelekwa kwingine, kuna utaratibu unaitakiwa kufuatwa wa kiofisi ambao ni kupitia barua na si kinyume cha hapo, huku akiwataka wafanye hivyo haraka ili kukamilisha zoezi hilo.
Akizungumza kwa niaba ya chama, Naibala alimshukuru Mkurugenzi huyo huku akisema kwamba kwa kipindi kifupi ambacho amefika ndani ya halmashauri hiyo kazi yake inaonekana.
"Tumeshuhudia taa katika eneo la Lugoba wanapokatia ushuru hatua inayolenga kunoreshwa kwa ukusa yaji, imani yetu ni kwamba hapo siku za baadae zitasambazwa kwani hazina gharama kutokana na kutumia nishati ya jua," alisema Naibala.

No comments:
Post a Comment