Maelfu ya raia wa Poland wameandamana jana kupinga kuanza kutekelezwa kwa uamuzi wa mahakama ya katiba unaozuia utoaji mimba kwenye taifa hilo lenye idadi kubwa ya wakristo wakatoliki.
Wanaandamanaji kwenye mji mkuu Warsaw waliwasha fashifashi nyekundu, kupeperusha bendera zenye rangi ya upinde wa mvua pamoja na mabango yanayolaani uamuzi huo wanaoutaja kuwa kinyume cha uhuru wa mtu kufanya maamuzi binafsi.
Mahakama ya Poland ilitoa uamuzi huo Oktoba 22 mwaka jana unaosema utoaji mimba kwa sababu ya hitilafu za maumbile yaa mtoto aliye tumboni ni kinyume na katiba.
Uamuzi huo unamaanisha kwamba itakuwa kosa kisheria kutoa mimba nchini Poland isipokuwa kwa wanawake waliobakwa au pindi itathibitika kwamba uhai wa mwanamke umo hatarini.
Serikali ya kihafidhina ya Poland ambayo imesema inaunga mkono uamuzi huo na itaupa nguvu ya kisheria kwa kuuchapisha kwenye jarida la sheria la taifa kama sehemu ya kutimiza wajibu wa kikatiba.

No comments:
Post a Comment