Search This Blog

Wednesday, January 27, 2021

Chanjo za Sinovac na Sinopharm kutoka China kuorodheshwa kwa matumizi ya dharura na WHO


Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limetathmini aina mbili mpya za chanjo za corona kutoka kwa kampuni za Kichina kwa ajili ya kujumuishwa kwenye "orodha ya matumizi ya dharura".

Katika ripoti iliyotolewa na televisheni ya mtandao ya China (CGTN), ilielezwa kuwa WHO ilichunguza data za chanjo ya Sinovac na Sinopharm kutoka China.

Ripoti hiyo ilifahamisha kwamba timu ilikuwa ikifanya kazi na kampuni kutathmini uzingatiaji wa mazoea ya utengenezaji wa ubora wa kimataifa kabla (chanjo) kujumuishwa katika orodha ya matumizi ya dharura na WHO.

China imefanya makubaliano na takriban nchi 24 kwa ajili ya usambazaji wa chanjo ya Sinovac na Sinopharm.

Makamu wa Rais wa Tume ya Kitaifa ya Afya ya China (NHC) Zıng Yishin alisema, "Mchakato wa chanjo unaendelea vizuri na idadi ya watu wanaohitaji kupewa chanjo inaongezeka."

Zing pia alisema kuwa watu walio katika hatari kubwa na wataalamu wa huduma za afya wanapewa kipaumbele katika utoaji chanjo.

Kesi mpya 75 za Covid-19 ziliripotiwa nchini China ndani ya masaa 24 yaliyopita na hakukuwa na vifo kutokana na virusi.

Nchi ya China ambayo ni chimbuko la Covid-19, imeripoti vifo vya watu 4,636 na kesi 89,272 za maambukizi ya virusi hadi kufikia sasa.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...