Watu 53 wameripotiwa kufariki na wengine 29 kujeruhiwa kutokana na ajali ya mgongano kati ya basi la abiria na lori katika mji wa Dschang nchini Cameroon.
Kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya ndani, basi lililokuwa limebeba abiria wapatao 70 liligongana na lori katika eneo la Falaise karibu na mji wa Dschang.
Kwa mujibu wa maelezo ya awali, watu 53 walipoteza maisha na wengine 29 walijeruhiwa kwenye ajali hiyo, ambapo magari yaliteketea kwa moto uliosababishwa na mgongano huo.
Maafisa wa utawala wanahofia uwezekano wa kuongezeka kwa idadi ya vifo.

No comments:
Post a Comment