Search This Blog

Friday, January 22, 2021

Biden aagiza kuvaliwa kwa barakoa , sheria mpya za usafiri dhidi ya corona


Rais wa Marekani Joe Biden ametilia mkazo sheria za kuvaa barakoa na kuagiza kuwekwa chini ya karantini kwa watu wanaosafiri kuelekea nchini humo wakati akianza kutekeleza majukumu yake katika kukabiliana na janga la virusi vya corona katika siku ya kwanza madarakani. 

Akitia saini maagizo 10 ya rais katika ikulu ya White House, Biden ameliambia taifa hilo kwamba idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa COVID-19 huenda ikaongezeka hadi nusu milioni kufikia mwezi ujao na kwamba hatua za dharura zinahitajika.

Biden amesema kuwa taifa hilo liko katika hali ya dharura na ni wakati wa kuichukulia hali nchini humo kuwa hivyo. 

Ameongeza kwamba anataka kurejesha imani ya umma baada ya utawala wa mgawanyiko wa Donald Trump. Biden amesema kwamba chini ya utawala wake, wanasayansi watafanya kazi bila kuingiliwa kisiasa na kuahidi kushauriana nao kila wanapokosea.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...