Leicester City wameacha mpango wao wa uhamisho kwa ajili ya kiungo wa kati wa Inter Milan Christian Eriksen, 28, kwasababu mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark anataka mshahara wa pauni 300,000-kwa wiki. (Telegraph)
Bayern Munich wamethibitisha haja yao ya kusaini mkataba na Mlinzi wa RB Leipzig Mfaransa Dayot Upamecano, mwenye umri wa miaka 22 ambaye katika mkataba wake ana kipengele cha kumuachilia cha thamani ya pauni milioni 40. (Mirror)
Manchester United, Manchester City na Chelsea kwa pamoja wameonesha nia yao katika ya kumtaka Dayot Upamecano, ambaye mkataba wake hautasainiwa hadi mimu ujao. (Goal)
Licha ya klabu mbali mbali kuonesha kumtaka kiungo wa kati wa Real Madrid Mnorway Martin Odegaard mwanye umri wa miaka 22, anakaribia kabisa kukamilisha uhamisho wake wa mkopo kuelekea Arsenal. (Sport - in Spanish)
Kiungo wa kati wa Crystal Palace raia wa Jamuhuri ya Ireland midfielder James McCarthy, 30, analengwa na klabu ya championi ya Uskochi Celtic. (Mail)
Arsenal wanataka kusaini mkataba na kiungo wa kati- kushoto Mskochi Kieran Tierney, 23, kabla ya kumalizika kwa dirisha la uhamisho wa wachezaji mwezi Januari. (Express)
West Ham huenda wakashusha bei yao wanayoitaka kwa kiungo wa kati wa Declan Rice, 22, hadi kufikia pauni milioni £50 kwasababu ya athari za janga la virusi vya corona. (90min)
Kiungo wa kati wa Tottenham na England Dele Alli, 24, amemuomba mwenyekiti Daniel Levy asimuwekee pingamizi katika uwezekano wke wa kuhamia Paris St-Germain. (90min)
Hammers wanajiandaa kuboresha dau la pauni milioni 16 kwa ajili mshambuliaji Mnorway wa Bournemouth Joshua King, 29. (Sun)
Hatahivyo, Burnley wamejiunga na West Ham na West Brom katika kinyang'anyiro cha kusaini mkataba na King, ambaye mkataba wake unakamilika msimu huu. (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Ecuador Moises Caicedo, 19, anatarajiwa kusafiri kuelekea England Ijumaa kukamilisha mkataba wa pauni milioni 4.5 wa kuhamia Brighton kutoka klabu ya Independiente del Valle. (Sky Sports)
Meneja wa Marseille Andre Villas-Boas amesema ofa kwa kiungo wa kati wa Aston Villa Morgan Sanson, 26, "inasikitisha". (Mail)
Meneja wa Real Sociedad Imanol Alguacil anatarajia kuwa na mshambuliaji wa Mbrazili Willian Jose, 29, wikendi, licha ya Wolves kumtaka. (Marca, via Birmingham Mail)
Mkurugenzi mtendaji wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge anasema hakuna fursa ya klabu ya kumuuza winga Mjerumani Leroy Sane, 25, licha ya kuonekana mara chache katika kikosi cha kwanza tangu alipohama kutoka Manchester City. (Manchester Evening News)
Wolves watatakiwa kulipa takriban pauni milioni 17 kumsaini Jose kwa mkataba wa kudumu. (Express & Star)
Kiungo wa zamani wa kati wa Manchester City na Ivory Coast Yaya Toure yuko tayari kuchukua hatua za kwanza katika kufundisha timu ya Uturuki ya Olympic Donetsk. (ESPN)
Manchester United wanashinda kinyang'anyiro cha kusaini mkataba na mbrazili Gabriel Veron, 18, ambaye anachezea safu ya mashambulio ya Palmeiras na ana kipengele cha pauni milioni 53 cha kumuachilia. (Sport, via FourFourTwo)
No comments:
Post a Comment