Jamuhuri ya Afrika ya Kati Alhamisi ilitangaza hali ya hatari ya siku 15 kufuatia jaribio la makundi yenye silaha kuuzingira mji Bangui katika juhudi za kumwondoa mamlakani Rais aliyechaguliwa tena Faustin Archange Touadera.
Katika tangazo kupitia redio ya taifa, msemaji wa ofisi ya rais Albert Yaloke Mokpeme amesema kuwa hali hiyo ya hatari imetangazwa kote nchini humo kuanzia saa sita usiku.
Mokpeme ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba hali hiyo ya hatari pia itaruhusu mamlaka ''kukamata watu bila kupitia waendeshaji mashtaka wa kitaifa.
' Tamko hilo la Alhamisi limekuja saa chache baada ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo kulitaka Baraza la Usalama kukubali "ongezeko kubwa" la idadi ya wanajeshi wa kudumisha amani nchini humo kukabiliana na ghasia mbaya.

No comments:
Post a Comment