Search This Blog

Friday, December 18, 2020

WHO kutuma wajumbe China kwa ajili ya utafiti wa Covid-19


Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) litatuma wajumbe kwenda China kuchunguza jinsi virusi vya corona (Covid-19) vilivyoanzia na kusambazwa kutoka kwa wanyama hadi kufikia wanadamu.

Fabian Leendertz ambaye ni mmoja wa wajumbe watakaopelekwa China na mtaalamu katika Taasisi ya Robert Koch nchini Ujerumani, alizungumza na wanahabari na kusema kuwa lengo la kupeleka wajumbe China ni kukusanya data ili kujiandaa vyema kwa magonjwa ya milipuko yajayo.

Leendertz alisema kuwa wanatarajia ziara hiyo iliyopangwa kufanyika mwezi ujao, kuanzia mkoa wa Wuhan nchini China, ambako Covid-19 iligundulika kwa mara ya kwanza.

Leendertz pia alisema kwamba wajumbe hao watachunguza ikiwa kuna data zozote za matibabu zinazoweza kudhihirisha endapo virusi hivyo vilikuwa vinasambaa mapema kuliko ilivyofikiriwa, kabla ya kesi ya kwanza kugundulika.

Akibainisha lengo la ziara hiyo ni kutatua kile kilichotokea Wuhan kwa ujumla, na chimbuko la virusi ni kwa mnyama gani haswa na namna vilivyofika kwa binadamu, Leendertz aliongezea kusema kuwa wataweza kutambua sababu zaidi za kuenea kwa janga hilo na hatua bora zitachukuliwa dhidi yake katika siku zijazo.

Virusi vya Covid-19 ambavyo vilitokea Wuhan China mnamo Desemba 2019, vilienea kwa zaidi ya nchi 200 na kugeuka kuwa janga kubwa. Wakati idadi ya kesi za maambukizi ikizidi milioni 74, zaidi ya watu milioni 1,657,000 walipoteza maisha kutokana na virusi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...