Search This Blog

Friday, December 18, 2020

Tetesi za Soka kimataifa


Manchester United huenda wakawasilisha dau la kumnunua kiungo wa kati wa West Ham Declan Rice, 21, japo mchezaji huyo anadhaniwa kutaka kujiunga na Chelsea endapo ataamua kuondoka Hammers. (Express)

Wolves inamfuatilia mshambuliaji wa Liverpool na Ubelgiji Divock Origi, 25, ambaye huenda akaruhusiwa kuondoka mwezi Januari. (Mail)

Manchester United wanashughulikia mchakato wa Marcos Rojo kuondoka klabu hiyo mwezi Januari, huku Newcastle wakipania kumsajili kwa mkopo mlinzi huyo wa Argentina aliye na umri wa miaka 30. (The Athletic - subscription required)

Liverpool wamemuongeza mchezaji Roma wa safu ya kati na nyuma Roger Ibanez katika orodha ya walinzi wanaosakwa kujaza pengo lililoachwa na mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi Virgil van Dijk, 29, aliyejeruhiwa na huenda wakawasilisha dau la £30m kumnunua Mbrazili huyo mwenye umri wa miaka 22. (AS Roma Live, via Team Talk)

Mgombea wa Rais wa Barcelona Victor Font amesema hatarudia makosa yaliyofanywa na watangulizi wake kutangaza nia ya kuwanunua wachezaji nyota licha ya kuhusishwa na tetesi za kumnyatia mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Haaland, 20. Lakini anapanga kumshawishi Lionel Messi, 33, kusaini mkataba mpya. (Goal)

Kiungo wakati wa Hungary Dominik Szoboszlai, 20, anayenyatiwa na Arsenal, amekamilisha uhamisho wa RB Leipzig kutoka klabu dada ya Red Bull Salzburg, na anatarajiwa kujiunga nayo mwezi Januari baada ya kusaini mkataba wa mika minne na nusu. (Mirror)

Arsenal inaonekana inakaribia kukamilisha usajili wa mchezaji wa safu ya kati na nyuma ya Hertha Berlin Omar Rekik baada ya mlinzi huyo aliye na umri wa miaka 18-year-kuwasili mjini London siku ya Alhamisi . (Metro)

Napoli itaitisha angalau £14m kumuuza mshambuliaji wa Poland Arkadiusz Milik mwezi Januari Januari licha ya mchezaji huyo kunyatiwa na Juventus na Atletico Madrid. Milik mwenye umri wa miaka 26-pia ananyatiwa na Everton. (Goal)

Mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti ana matumaini ya kukamilisha mkataba wake katika klabu hiyo kwa "ushindi wa mataji na kitu spesheli" katika kipindi cha muda atakaokuwa hapo hadi mwisho wa msimu wa 2023-24. (Liverpool Echo)



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...