Search This Blog

Wednesday, December 23, 2020

Wachimbaji wamadini ya dhahabu (Botana)Mrito waiomba serikali kuingilia kati mgogoro uliopo


Na Timothy Itembe MARA.

Wachimbaji wa madini ya dhahabu Botana uliopo Kijiji cha Mrito kata ya Kemambo wilayani Tarime mkoani Mara wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro uliopo baina yao na mmiliki wa Leseni.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wachimbaji hao walisema kuwa kwa nafasi yao wanatafiti maeneo ya kuchimba dhahabu huku wakitumia gharama za utafiti chini makubaliano ya mdomo ya mwenye Leseni Mwita Masyaga lakini cha kushangaza wanapokuwa wamefanikiwa na kuanza kutoa mali mwenye leseni anawageuka akihitaji kuwasainisha mikataba kandamizi hali ambayo inasababisha kukwama na mwenyeleseni kuwafungia mashimo.

Saidi Mbuya mchimbaji mdogo ambaye pia ni mdhamini wa wachimbaji alibainisha kuwa mmiliki wa Leseni hana mwonekano wa kusaidia wachimbaji wanaokuwa wamebaini madini badala yake anataka kunufaika peke yake na falimia yake huku akiwaacha walioanzisha mashimo wakiendelea kuteseka.

Mbuya aliomba serikali kuingilia kati sakata hilo ikiwa ni pamoja na Waziri wa madini kuja kwa lengo la kusaidia kero hiyo ambapo atafika na wataalamu wa kutafsiri sheria inasamaje baina ya mmiliki wa leseni,mchimbaji na mwenye eneo wanagawanaje mali pindi inapokuwa imepatikana hususani madini ya dhahabu.

Naye Rimo Marwa alisema kuwa wachimbaji hao walianza kazi ya kufukua shimo hilo linalojulikana kama la mkoloni (Botana) mwezi 8,tarehe 20 mwaka huu ambapo tulifanikiwa kupata dhahabu na mwenye leseni akaja juu ili kutusimamisha mikataba kandamizi hali ambayo ilizua mgogoro nasisi kuchukua hatua ya kuwaona viongozi wa madini ili kuja kuangalia na kutoa muongozo hadi habari hizi zinatangazwa viongoi hao hawajafika.

Kwa upande wake Matinde Koroso alisema kuwa baada ya kutokea stofahamu wakina mama wamekwama katika shuguli ya uzalishaji badala yake wanarandaranda mitaani bila kazi na watoto wanateseka majumbani bila chakula na matumizi mengine kwa hali hiyo wanaiomba serikali kuingilia kati wafunguliwe masimo na wakaanze kazi ya uzalishaji.

"Mimi kama mwana mama kufungiwa mashimo na mwenye Leseni Mwita Masyaga kumetusababisha watoto wetu kulala njaa hali kwetu hapa Nyamongo kazi yetu kubwa tunategemea kuzalisha kupitia machimbo,kilimo na mifugo ambapo mifugo kwa sasa hatuitegemei sana kutokana na wizi kushamiri na kilimo ni cha kubahatisha kwa hali hiyo tunaomba Rais wetu John Pombe Magufuli na Waziri wake watusikie kilio chetu wakina mama wajasilia mali wadogo watusaidie"alisema Koroso.

Wakati huo huo Afgisa mtendaji wa kijiji cha Mrito,Protas Visent alithibitisha wananchi wake kusumbulia na mwenye leseni ambapo anawasainisha mikataba kandamizi bila ya makubaliano yao ambapo alitumia nafasi hiyo kuitaka serikali kumshauri kukaa vizuri na wenye mashimo vinginevyo serikali imnyanganye leseni.

Afisa huyo aliongeza kusema kuwa baadhi ya vipengele kandamizi vilivyopo kwenye mikataba ni pamoja na kipengele namba mbili kinachosema kuwa mawe,mtete au chochote kabla wakati au baada ya utafiti kimepatikana utaratibu wote mpaka kupata dhahabu ufanyike kwewnye mwalo wa mwenye leseni.

Pia aliongeza kipengele kingine ni pamoja na kipengele namba 3 kinachosema kuwa mawe mtete au chochote kitakachopatikana iwe wakati wa utafiti au uchimbaji kwa kila viroba kumi(10) baada ya kuponda mwenye leseni atachukua viroba vinne(3) na wanachama viroba sita(7).



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...