Urusi imetuma askari wa ziada 300 wa mafunzo katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati (CAR) kukabiliana na kile Wizara ya mashauri ya kigeni ya nchi hiyo imesema "kushuka kwa kiwango cha usalama kwa hali ya juu ".
Inasema serikali ya CAR , ambayo inatishiwa namakundi ya waasi kabla ya uchaguzi wa Jumapili wa urais, ilikuwa imeomba usaidizi.
Naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Mikhail Bogdanov amesema kuwa wanajeshi wa Urusi hawahusiki katika mapigano katika CAR na kwamba watoa wakufunzi wa kijeshi "sio wanajeshi wala kikosi maalumu".

No comments:
Post a Comment