Search This Blog

Wednesday, December 23, 2020

Maelfu waandamana Armenia wakimtaka waziri mkuu ajiuzulu


Wafuasi wa upinzani nchini Armenia jana wameandamana katika mji mkuu wa Yerevan, wakimtaka waziri mkuu ajiuzulu, kutokana na jinsi alivyoshughulikia mzozo wa Nagorno-Karabakh na nchi jirani ya Azerbaijan.

Wanasiasa wa upinzani na wafuasi wao wanamtaka Nikol Pashinyan ajiuzulu kufuatia makubaliano ya amani ya Novemba 10 ambayo yaliipa Azerbaijan udhibiti wa sehemu kubwa ya jimbo la Nagorno-Karabakh na maeneo ya karibu. 

Makubaliano hayo yaliyosimamiwa na Urusi yalimaliza siku 44 za mapigano makali, ambayo jeshi la Azerbaijan ilivishinda vikosi vya Armenia. 

Maelfu wa waandamanaji walishiriki katika maandamano na wengine kuvamia majengo ya serikali. Viongozi wa maandamano hayo wanasema waandamanji watapiga kambi kwenye uwanja mkuu wa Yerevan hadi waziri mkuu Pashinyan atakapoondoka madarakani.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...