Umoja wa Ulaya leo Jumamosi umeanza mpango wa kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 licha ya baadhi ya nchi za Umoja huo kusitisha shughuli zao za kiuchumi ili kudhibiti kusambaa kwa aina mpya ya kirusi cha Corona ambacho kilizuka hivi karibuni nchini Uingereza na ambacho kinaaminika kuenea kwa kasi zaidi.
Waziri wa afya wa Ufaransa amesema kuwa nchi hiyo imethibitisha mtu wa kwanza nchini humo aliyepatikana na aina mpya ya kirusi cha Corona, ambaye ni raia wa Ufaransa aliyerudi nchini humo akitokea Uingereza.
Tayari nchi kadhaa zimeripoti kugundua aina mpya ya kirusi cha Corona na kuzua taharuki kwa mfumo wa afya ambao tayari umelemewa kutokana na ugonjwa wa Covid-19.
Janga la virusi vya Corona limesababisha vifo vya zaidi ya watu milioni 1.7 kote duniani, lakini mpango wa utoaji chanjo uliozinduliwa hivi karibuni umeleta matumaini kuwa ugonjwa huo utatokomezwa licha ya kuibuka kwa aina mpya ya kirusi cha Corona.

No comments:
Post a Comment