Na, Baraka Messa Songwe.
TIMU ya soka ya Insipire ya Vwawa wilayani Mbozi imeanza vema mashindano ya ligi ya mkoa wa Songwe hatua ya sita bora kwa kuifunga timu ya Effort kutoka Tunduma juzi kwa jumla ya goli 2-0.
Katika pambano Hilo lililokuwa na upinzani mkubwa iliwalazimu Insipire kusubiri mpaka dakika ya 54 ambapo ndipo walijipatia bao lao la Kwanza kupitia kwa Juma Shebu aliyetokea benchi.
Shebu alifunga goli hilo baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Effort na kumpiga chenga goli kipa Kisha kutumbukiza mpira nyavuni.
Baada ya goli Hilo Effort walibadilika na kuanza kushambulia kwa nguvu lango la wapinzani wao, lakini uimara wa safu ya ulinzi wa timu ya Insipire ulitulia na kuondoa hatari zote golin kwao.
Zikiwa zimebakia dakika mbili mpira kumalizika Insipire walio onekana wametulia na kucheza kitimu zaidi walijipatia goli la pili baada ya kushambulia kwa kushitukiza na kupata faulo ambayo ilimaliziwa na Isaya Wega baada ya kumalizia mpira uliogonga mwamba na kurudi uwanjani hivyo kumkuta mfungaji aliye funga kirahis.
Kwa matokeo hayo Insipire wanapanda kileleni kwa kujikusanyia hizo point tatu muhimu huku timu za Bandar na Holywood zikifuatia kwa kuwa kuwa na point mojamoja.
Ligi hiyo iitaendelea Tena leo jion desemba 26 kwa timu za Mapinduzi ya Hasamba Mbozi kukutana dhidi ya timu ya Itumba stars kutoka Ileje.

No comments:
Post a Comment