Search This Blog

Tuesday, December 22, 2020

Mahakama ya Kosovo yaamrisha uchaguzi mpya


Mahakama ya kikatiba ya Kosovo imetoa uamuzi hapo jana ambao utalazimisha kufanyika uchaguzi mpya nchini humo. 

Jaji aligundua kuwa uchaguzi uliompa ushindi waziri mkuu wa sasa, Avdullah Hoti, mnamo Juni 3 ulikiuka sheria. 

Hoti alichaguliwa kwa idadi ndogo ya kura 61 kati ya wabunge 120. Uamuzi huo mpya wa mahakama unasema kuwa uchaguzi wa Hoti haukuwa halali, kwa sababu mmoja wa wabunge waliompigia kura hakustahiki kufanya hivyo. 

Mwanasiasa huyo alikuwa amekutwa na hatia ya kosa la udanganyifu wakati wa kupiga kura. Mwishoni mwa mwezi Septemba, alianza kutumikia kifungo chake gerezani.

 Rais wa sasa, Vjosa Osmani, atakutana na wawakilishi wa chama leo kuamua tarehe mpya ya uchaguzi, kulingana na ripoti za vyombo vya habari. Uchaguzi mpya lazima ufanyike ndani ya siku 40.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...