Search This Blog

Tuesday, December 22, 2020

Alikiba atangaza kuachia album yake mpya

 


Nyota wa muziki nchini, msanii Alikiba, ameweka wazi kuwa ataachia album yake mpya mapema mwaka 2021.

Kiba ameeleza hayo akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM jana, ambapo amesema mara ya mwisho kutoa album ilikuwa ni mwaka 2008.

"Mara ya mwisho kutoa album ilikuwa 2008. Mwakani 2021, nitatoa tena album, haitofika mwezi wa sita." amesema Alikiba ambaye ni boss wa lebo ya Kings Music.

Kwa kauli hiyo ya Kiba, anaungana na msanii Jay Dee ambao wote washatoa ahadi kwa mashabiki wao ya kuachia album mwakani.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...