Search This Blog

Tuesday, December 22, 2020

Jeshi la Azerbaijan lapoteza mashujaa 2,802


Jeshi la Azerbaijan lilipoteza wanajeshi mashujaa 2,802 katika operesheni iliyofanyika Nagorno-Karabakh kukomboa wilaya zake kutoka kwa uvamizi.

Wizara ya Ulinzi ya Azerbaijan ilitoa upya taarifa juu ya idadi ya waliopoteza maisha kwenye mapigano yaliyoanza mnamo Septemba 27 na kumalizika Novemba 10 baada ya makubaliano kutiwa saini kufuatia kukubali kushindwa kwa Armenia.

Katika taarifa iliyotolewa, iliarifiwa kuwa idadi ya wanajeshi mashujaa waliofariki, ambayo hapo awali ilitangazwa kuwa 2,783, iliongezeka hadi kufikia 2,802 baada ya ugunduzi wa makaburi kadhaa na vitambulisho vyao.

Taarifa hiyo pia ilieza kuwa zaidi ya wanajeshi mashujaa 60 waliouawa bado hawajatambuliwa, na kufahamisha kuendelezwa kwa juhudi za kuwatambua na kuwapata wanajeshi 40 walipotea.

Wizara hiyo pia ilichapisha orodha ya wanajeshi mashujaa waliouawa na kuzikwa kwa umma.

Baada ya ukombozi wa vituo vya miji 5, wilaya 4 na vijiji 286 katika operesheni iliyozinduliwa na jeshi la Azerbajain mnamo Septemba 27, Armenia ilikubali kushindwa na kutia saini makubaliano ya kuahidi kuhamisha maeneo ya Aghdam, Lachin na Kelbajar.

Jeshi la Armenia liliondoka Aghdam mnamo Novemba 20, kutoka Kalbajar mnamo Novemba 25 na kutoka Lachin mnamo Desemba 1.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...