Search This Blog

Tuesday, December 22, 2020

Joe Biden na mkewe wapewa chanjo ya corona


Rais mteule wa Marekani, Joe Biden jana Jumatatu amepokea chanjo dhidi ya virusi vya corona wakati akitazamwa moja kwa moja kwenye televisheni ili kushawishi Wamarekani kuwa zoezi hilo ni salama.

Kabla ya kupokea chanjo hiyo, Biden alionekana akijiandaa na kisha kumweleza muuguzi kuendelea na shuguli wakati akiwa kwenye hospitali moja mjini Newark, Delaware.

Mkewe Jill Biden saa kadhaa kabla pia alipokea chanjo kwenye hospitali hiyo ambayo iko karibu na makazi yao.

Baadhi ya viongozi wengine mashuhuri wa Marekani waliopokea chanjo hiyo tayari ni pamoja na makamu wa rais Mike Pence, Spika wa bunge Nancy Pelosi na kiongozi wa walio wengi kwenye baraza la Senate Mitch McConnell.

Marekani inaongoza ulimwenguni kwenye idadi ya maambukizi huku tayari ikiwa imeshuhudia zaidi ya vifo 318,000 kutokana na Covid-19 kwa mujibu wa takwimu za chuo kikuu cha Johns Hopkins.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...