Search This Blog

Wednesday, December 30, 2020

EU kusajili wanaokataa chanjo ya Covid-19


Nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU) ambazo zimepewa uhuru wa matumizi ya chanjo dhidi ya janga la corona (Covid-19), lakini pia wale wanaokataa kufanyiwa chanjo hiyo watasajiliwa.

Waziri wa Afya wa Uhispania Salvador İlla alizungumza na kituo cha televisheni cha La Sexta nchini humo na kusema kuwa wale ambao hawatafanyiwa chanjo ya Covid-19, watasajiliwa na data hizo zitasambazwa kati ya taasisi rasmi za EU.

"Tunachotaka ni raia waitike wito wa kufanyiwa chanjo dhidi ya Covid-19. Wale ambao wanakataa chanjo hiyo watasajiliwa na data hizo zitasambazwa kati ya wanachama wa EU. Rekodi zao hazitosambazwa kwa umma kwa kuzingatia ulinzi na usalama wa data za kibinafsi."

Wakati huo huo, nchini Uhispania kumekuwa na majadiliano ya kisiasa yanayoendelea juu ya uundaji wa mifumo ya kidigitali ya kuhifadhi data ambapo data za watu watakofanyiwa chanjo zitakusanywa kwenye "kadi ya chanjo ya Covid-19", "pasipoti ya chanjo ya Covid-19" au "Cheti cha elektroniki cha Covid-19".

Utawala huru wa Madrid na Andalusia ulitangaza kuwa kadi ya chanjo ya kidigitali itatolewa kwa raia wanaohusiana na Covid-19 haraka iwezekanavyo.

Kadi za chanjo ya Covid-19 zinaarifiwa kwamba zitaweza kutumika haswa katika mazingira ya usafiri na biashara.

Baadhi ya kampuni za Uhispania pia zinadaiwa kuanzisha mchakato wa kusitisha mikataba ya wafanyikazi wao ambao wanakataa kufanyiwa chanjo ya Covid-19.

Shirika la Afya Ulimwenguni pia linafahamika kufanya utafiti juu ya kadi za kidigitali za Covid-19.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...