Maafisa wa wanyama pori wamesambaza picha za nyoka mwenye macho matatu aliyepatikana katikati ya barabara kaskazini mwa Auustralia.
Shirika la huduma kwa wanyama pori na bustani za wanyama Northern Territory Parks and Wildlife Service wameeleza kwamba nyoka huyo ambaye picha zake zilisambaa pakubwa katika mitando ya kijamii, ni wa "kustaajabisha".
Amepewa jina la Monty Python, hatahivyo nyoka huyo aina ya chatu alifariki wiki kadhaa tu baada ya kugunduliwa .
Wataalamu wanasema jicho la tatu la nyoka huyo lililo juu ya kichwa chake limeonekana kuwa ni mabadiliko ya asili
Maafisa walimgundua nyoka huyo katika mji wa Humpty Doo, 40km kusini mashariki mwa Darwin.
Ana urefu wa 15 inchi na alikuwa akipata tabu kula chakula kutokana na ulemavu wake, maafisa wameiambia BBC.
Shirika hilo la huduma kwa wanyama pori limesema picha za X-ray zimeonyesha kwamba hakuwa na vichwa viwili kwa pamoja.
"Badala yake alionekana kuwa na fuvu moja la kichwa na jicho la ziada ukijumlisha, macho matatu yanayofanya kazi sawasawa," lilieleza kwenye Facebook.

No comments:
Post a Comment