Kampuni ya Dawa ya Shanghai Fosun (Fosun Pharma) kutoka China imetia saini makubaliano ya ununuzi wa dozi milioni 100 za chanjo ya corona (Covid-19) iliyozalisha na kampuni ya Ujerumani ya bioteknolojia ya BioNTech iliyoanzishwa na mwanasayansi wa Kituruki Prof. Dk. Uğur Şahin kwa ushirikiano.
Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na kampuni hizo, iliarifiwa kwamba makubaliano yalitiwa saini kwa ajili ya ununuzi wa dozi milioni 100 za kwanza kwa China za chanjo inayoitwa BNT162, iliyozalishwa kwa teknolojia ya mRNA dhidi ya Covid-19.
Maelezo yaliyotolewa pia yalikumbusha kuwa Kampuni ya Dawa ya Shanghai Fosun na kampuni ya BioNTech iliwahi kutangaza mpango wa kushirikiana na China katika maendeleo na vipimo vya kliniki na uuzaji wa chanjo ya Ujerumani aina ya "BNT162" mwezi Machi, na kusaidia shughuli ya usambazaji.
Mnamo tarehe 24 Novemba, kampuni hizo pia zilitangaza kuanzisha majaribio ya kliniki ya hatua ya 2 nchini China kwa chanjo iliyozalishwa dhidi ya Covid-19.

No comments:
Post a Comment