Mahakama nchini Ufaransa umewahukumu watu 14 hukumu ya kifungo cha kati ya miaka 4 hadi maisha gerezani kwa kuhusishwa na shambulizi la kigaidi la 2015 la jarida la tashtiti la Charle Hebdo.
Miongioni mwa 14 hao yupo alietajwa kuwa mshtikiwa mkuu Ali Riza Polat, ambaye amekutwa na makosa kuyapanga mashambulizi hayo na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani, Kijana wa umri wa miaka 35, mwenye asili ya Kifaransa na Kituruki amekutwa na hatia ya kusaidia na kuchochea uhalifu wenye dhamira ya kigaidi ikiwa na miongoni na mashitaka mengine pia amehukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani.
Polat, ambae mara zote amekuwa akikanusha tuhuma hizo alisikika wakati wa hukumu akisema kwa sauti kwamba hicho kilichosemwa ni uongo. Lakini wote hao walikuwa katika mashtaka hayo walihusishwa kwa kutoa misaada kwa wahalifu kwa kuwapa misaada au vifaa kama gari. Aidha katika hukumu hiyo pia, mahakama iliweza kuyatupilia mbali mashtaka kadhaa ambayo dhidi ya watumiwa ambayo yaliwasilishwa na waendesha mashtaka.
Watuhumiwa watatu wahukumiwa bila ya kuwepo mahakamani
Hukumu hiyo inawahusu pia watuhumiwa watatu ambao inadaiwa walikimbilia katika mamalaka ya Kundi la Dola la Kiislamu nchini
Syria, ikiwa ni muda mfupi tu baada ya kufanyika kwa tukio hilo la mauwaji la Paris, ambapo watu 17 walipoteza maisha.
Kwa mujibu ya wachunguzi nchini Ufaransa zipo hisia za ndugu wawili miongoni mwa watatu hao Mohammed na Mehdi Belhoucine wamekufa ingawa Mohammed alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani. Richard Malka, ni mwanasheria analiwakilisha jarida la Charlie Hebdo "Kinachonivutia ni kwamba, ujumbe umetolewa kwa jamii na ujumbe huu ni kwamba yeyote atakaewasaidia magaidi namna moja au nyingine ana ya hatari ya kukabiliwa na hukuma kali."
Ali Riza anatazwamwa kama mtu wa karibu sana na muuaji Amedy Coulibaly
Kwa zingatio la hukumu iliyotolewa, kituo kimoja cha radio cha umma France International, kimemnukuu mtoa hukumu, Jaji Mfawidhi Regis de Jorna akisema "Mahakama imegundua Polat alishiriki kwa kiwango kikubwa na kwa namna ya kimfumo kutekeleza uovu."
Lakini hata hivyo wengi wa hao wameshindwa kujiepusha na mashtaka ya kushiriki biashara haramu ya silaha na dawa za kulevya. Polat anatazwamwa kama mtu wa karibu sana na muuaji Amedy Coulibaly, ambaye alimuuwa kwa kumpiga alimpiga risasi polisi na baadae pia kuwauwa kuwaua watu wanne waliochukiwa mateka katika duka kubwa ikiwa ni baada ya shambulio kwenye jarida hilo la Charlie Hebdo ambalo kwa wakti huo liliingia katika lawama kwa kuchapisdha katuni zinazomdhihaki mtume Mohammed.
Hata hivyo nae Coulibaly aliuawa na polisi ambao walivamia na kulishambulia duka la vyakula ambalo ilihisiwa kuwa alikuwemo katika mkasa huo wa 2015.

No comments:
Post a Comment