Search This Blog

Wednesday, December 16, 2020

Ofisa Mipango Wilaya ya Kibaha atakiwa kujipanga


Na Omary Mngindo, Mlandizi

OFISA Mipango na Wataalamu wake Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani, wametakiwa kujipanga kuhakikisha wanatumia fursa ya Reli ya Mwendokasi inayopita maeneo hayo.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Erasto Makala, akizungumza kwenye uzinduzi wa Baraza la Madiwani, ambapo alisema wana-Kibaha wana kila sababu ya kunufaika kupitia mradi huo mkubwa.

"Ndani ya Halmashauri yetu mradi huu umeanzia Ngeta Stesheni, Kikongo, Ruvu, Kwala na Magindu, pale Kwala tuna mradi wetu wa viwanja, tuchangamkie kuviandaa kuusubiri mradi wa Bamdari kavu," alisema Makala.

Aliongeza kwamba mradi huo una maeneo makubwa mawili, ambayo no Ngeta na Kwala hivyo no vema wakajenga vitega uchumi vitavyoipatia halmaahauri mapato yatayotumika kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

"Kuhusu hali zetu za barabara, tutakaa na wenzetu wa TARURA ili kuona ni namna gani tunavyoweza kuziweka katika mazingira mazuri, nakumbuka Mbunge alipokuwa katika Kampeni alikuwa anazungumzia mikakati ya Kibaha kuwa Mji," alisema Mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Michael Mwakamo aliwataka Madiwani na Wataalamu kushirikiana kutatua kero zinazowakabili wananchi, huku akisisitiza kutumika kwa Waandishi wa habari kutangaza kazi zinazofanyika.

"Rais wetu Dkt. John Magufuli anafanyakazi kubwa pengine kushinda hata za nje ya mipaka yetu, lakini tunazisikia kutokana na kuwatumia Waandishi, hapa kwetu tatizo nini? Nataka tuwatumie watangaze kazi zinazotekelezwa na Magufuli," alisema Mwakamo.

Awali Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Butamo Ndalahwa aliwaambia Madiwani hao kuwa, kuna mikakati mbalimbali imeandaliwa kwa kushirikiana na wataalamu, na kwamba kwakuwa waneshachaguliwa wataendelea kuijadili kupitia vikao hivyo 




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...