Akikabiliwa na maandamano makubwa ya umma kumtaka ajiuzulu, Waziri Mkuu wa Armenia amewasilisha kile anachosema ni mpango wa kuhakikisha utangamano wa kidemokrasia, ili kuutatua mzozo wa kisiasa kufuatia hatua ya serikali yake kusaini mkataba wa kusitisha mapigano na Azerbaijan juu ya jimbo linalotaka kujitenga la Nagorno-Karabakh.
Maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana kila siku katika mji mkuu wa Armenia, Yerevan, wakimtaka Waziri Mkuu Nikol Pashinian aondoke madarakani.
Pashinian aliwaambia wafuasi wake wapatao 3,000 hapo jana kwamba anabeba dhamana ya mapungufu yote yaliyotokea, lakini anataka kubakia ili kusahihisha mambo.
Mkataba huo uliosimamiwa na Urusi ulifanikiwa kusitisha mapigano ya wiki sita ambayo yaliuawa maelfu ya watu, lakini yakaiamuru Armenia kurejesha baadhi ya maeneo iliyokuwa ikiyashikilia nje ya mipaka ya Nagorno Karabakh kwa Azerbaijan, sharti ambalo limewakasirisha wengi nchini Armenia.
Waziri wa Afya Arsen Torosian alisema hapo jana kuwa idadi ya wanajeshi wa Armenia waliokufa kwenye vita hivyo ni 2,425, likiwa ni ongezeko la 1,000 zaidi kuliko wale waliotajwa awali.

No comments:
Post a Comment